Genesis 17:1-6

Agano La Tohara

1 aAbramu alipokuwa na miaka tisini na tisa, Bwana akamtokea akamwambia, “Mimi ndimi Mwenyezi Mungu;
Mwenyezi Mungu hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).
enenda mbele zangu na uishi kwa unyofu.
2 cNami nitafanya Agano langu kati yangu na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.”

3 dAbramu akaanguka kifudifudi, naye Mungu akamwambia, 4 e“Kwa upande wangu, hili ndilo Agano langu na wewe: Wewe utakuwa baba wa mataifa mengi. 5 fJina lako hutaitwa tena Abramu, bali jina lako litakuwa Ibrahimu,
Ibrahimu maana yake Baba wa watu wengi.
kwa maana nimekufanya wewe baba wa mataifa mengi.
6 hNitakufanya uwe na uzao mwingi sana, kwako yatatoka mataifa nao wafalme watatoka kwako.
Copyright information for SwhKC